Jorafra Transport Agency Ltd inatangaza nafasi za ajira kwa waombaji wenye sifa stahiki kama ifuatavyo:
1. Usajili wa Leseni za Bajaji na Pikipiki
Mkoa wa Mwanza – Nafasi 25
- Kwimba – 5
- Misungwi – 5
- Sengerema – 5
- Magu – 5
- Buchosa – 5
Mkoa wa Dar es Salaam – Nafasi 15
2. Afisa Masoko (Marketing Officer)
Maeneo: Dar es Salaam na Arusha
Idadi: 1 kila mkoa
Mahitaji ya jinsia na umri: Kiume, miaka 22–30
Sifa za Mwombaji
- Awe Mtanzania na mkazi wa eneo husika.
- Ajue maeneo mengi ya mkoa husika.
- Elimu: Diploma au zaidi katika fani husika, Business Administration, au Logistics.
- Uzoefu wa kazi: Angalau miaka 2 katika sekta ya Logistics au Masoko.
- Kwa waombaji wa usajili wa leseni za pikipiki na bajaji,awe na simu janja na ajue kutumia kwa matumzi ya internet.
- Kigezo cha Elimu wa wanaosajili leseni iwe ni kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
Maelekezo kwa Waombaji Wote
- Waandike barua ya maombi kwa mkono kisha wa-scan bila watermark.
- Waambatanishe:
- Barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa.
- CV (Wasifu binafsi).
- Tuma barua zote ziandikwe kwa anuani:
Meneja Rasilimali Watu
Jorafra Transport Agency Ltd
S.L.P 735 Mwanza
Kisha zitumwe Kwa barua pepe: vacancy@jorafra.co.tz
Muda wa Maombi
- Kuanza kupokelewa: 05/04/2026
- Mwisho wa kupokelewa: 15/04/2026
Wito
Wote wenye nia na sifa stahiki wanakaribishwa kuwasilisha maombi yao kwa wakati.
ONYO:
Nafasi hizi ni za wazi na zinatolewa kwa mwenye sifa zilizotajwa pekee,usitoe wala kushawishi kwa pesa kupata nafasi tajwa.