Sio chakula tu ni upendo unaogawanywa, tabasamu linalozaliwa, na thawabu isiyo na kipimo.

Katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, Smile With Me Foundation inakualika kushiriki katika safari ya kutoa furaha na matumaini kwa watoto. Kupitia kampeni ya Iftar Charity 2026, tunalenga kuhakikisha kila mtoto anapata:

• 🥘Chakula cha futari cha kuwapa nguvu na furaha wakati wa kufuturu.

• 🧼 Vifaa vya usafi kwa maisha yenye afya na heshima.

• 📚 Vifaa vya shule ili kuendeleza ndoto na elimu bora.

Kwa nini tujitolee?

• Kila mchango wako ni dua iliyojibiwa kwa mtoto anayehitaji msaada.

• Kila sahani ya futari ni tumaini jipya kwa maisha bora.

• Kila tabasamu la mtoto ni thawabu yako mbele ya Mwenyezi Mungu.

👉 Changia sasa kupitia akaunti zilizotolewa kwenye poster rasmi ya kampeni.

🤍 Kwa pamoja, tunaleta tabasamu na tunagusa maisha.


Hashtags Rasmi

#SmileWithMeFoundation #SmileIftar #IftarCharity2026 #GusaMaisha #RamadhanNaSmile #ThawabuNiKubwa